Mwanamuziki mkongwe wa Hip Hop, Chid Benz amemtaka Godzillah kupunguza maneno yasiyo ya msingi kwenye nyimbo zake na badala yake afanye muziki mwepesi utakao burudisha watu na siyo kuandika kizungu kingi kinachompotezea mashabiki.

Chid amesema kwamba Godzillah alikuwa muandishi mzuri wakati anaingia kwenye game lakini kwa sasa amekuwa muandishi anayeandika vitu vingi kupitiliza kitu ambacho kinamfanya aonekane kama mtu asiyejua anataka nini kwenye uandishi wake.

Vile vile Chid ameongeza kwamba “Godzilla sasa hivi nyimbo zake za zina maneno mengi kiasi kwamba unaweza kuimba halafu ukasahau mwanzo ulikuwa unaimba nini”.

Kwa upande wa Wakazi na Billnass, Chid amewataka wasanii hao wapige kazi na kuachana na Godzilla kwani amekuwa mzungumzaji kuliko vitendo.

Hivi karibuni kumekuwepo na bifu linalomuhusisha msanii Godzilla pamoja na Wakazi huku msanii Billnass akitajwa kama mtu anayempatia Zilla changamoto katika muziki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *