Baada ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya mkali wa hip hop Bongo, Chidi Benz amefunguka na kusema kuwa ameamua kujikita kwenye killimo akishirikiana na mama yake mzazi ili kuweza kujikimu kimaisha.

Chid amesema kwamba mama yake ni mtu wake wa kwanza kwenye kumpatia sapoti ndiyo maana anashirikiana naye katika kuwajibika kiuchumi.

Mkali huyo amesema kuwa “Kwa sasa najishughulisha na kilimo kwa sana. Mimi na mama yangu tuna mashamba huko Chanika kwa hiyo hichi kipindi nilichokaa nje ya ‘game’ kilimo kinaendeleza maisha yetu japokuwa mimi mkulima wa mjini’.

Pia amesema kuwa “Lakini nina familia niliyoitengeneza kipindi nafanya vizuri kwenye game kwa hiyo siwezi nikafa na njaa wakati mimi nilikuwa nawalea na kuwasaidia pale walipokuwa wakinihitaji.

Ameongeza kwa kusema kuwa Wasanii wengi wapo upande wangu hawakumbuki mabaya yangu wengi wanarudisha mawazo yao nyuma kwa mazuri yangu”.

Hata hivyo rapa huyo kwa sasa amerudi na ngoma aliyomshirikisha Mkongwe Q- Chillah inayokwenda kwa jina la muda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *