Klabu ya West Ham United imekamilisha usajili wa mshambuliaji Javier Hernandez kutoka klabu ya Bayer Leverkusen kwa kiasi cha pauni milioni 16.

Mshambuliaji huyo raia wa Mexico alifika jijini London jana na kufanyiwa vipimo vya afya na amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo.

Hernnandez atakuwa analipwa mshahara wa pauni 140,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa kiasi kikubwa cha fedha katika historia ya klabu hiyo.

Chicharito aliibuka kuwa mfungaji bora zaidi wa Mexico katika historia baada ya kufunga bao lake la 47 mwezi Mei katika michuano ya kombe la mabara.

Mchezaji huyo ameifungia klabu ya Bayer Leverkusen mabao 39 katika mechi 76 alizoichezea timu hiyo inayoshiriki katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *