Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Cheyo amesema jukumu la viongozi wastaafu ni kuwaweka pamoja watanzania na siyo kuwafarakanisha kwa tofauti za kisiasa, kidini na uchama.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitambulisha ofisi za chama hicho zilizohamia Mwananyamala A jijini Dar es salaam.

Cheyo amesema anashangazwa na mawaziri wakuu wastaafu ambao walihamia upinzani na kuanza kutoa kauli ambazo kwa namna moja au nyingine zinaharatarisha amani.

Cheyo amesema kuingiza mambo ya dini katika siasa ni kutafuta mfarakano baina ya  wananchi na kwamba kwa maoni yake kiongozi ambaye ameshika nafasi kubwa kama Waziri Mkuu hatarajiwi kuliingiza taifa katika mafarakano.

Cheyo amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Rais wa awamu ya tano, Mh Dkt. John Magufuli na kuijenga Serikali imara, yenye kulinda maslahi ya nchi na ustawi wa watu wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *