Kamati ya pili kuhusu mchanga wa madini imewataja Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Sengerema, Wiliam Ngeleja kuhusu mikataba ya madini iliyoingiwa miaka iliyopita.

Mbali na hao pia imewaibua marehemu Dk Abdallah Kigoda aliyekuwa Mbunge wa Handeni na Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Majina ya viongozi hao yameibuka leo wakati  mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Nehemiah Osoro alipokuwa akiwasilisha matokeo ya ripoti yake.

Viongozi hao wametajwa kuhusika na mikataba hiyo ya madini wakati wa kipindi cha nyuma wakati wakiwa mawaziri wa Nishati na Madini.

Kamati hiyo imebaini kuwa kampuni ya Acacia haina usajili wa kufanya shughuli za uchimbaji wa madini hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *