Mwanamuziki wa hip hop, Chemical amesema kila anapokumbuka kifo cha mama yake anajikuta akilia sana kutokana na kutamani angeyaona mafanikio yake ya sasa kupitia muziki wake.

Chemical amesema hayo kutokana na mafanikio yake kwenye muziki ambapo mama yake hakuyaona mafanikio ya mtoto wake.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa inamuuma sana akikumbuka maisha ya nyuma ya mama yake japokuwa hakuishi nae.

“Sikulelewa na mama yangu kwa asilimia kubwa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua, lakini nilipotimiza miaka mitatu nikaambiwa niende Dar es Salaam kumsalimia, nilifika na furaha kumbe ndiyo alikuwa amefariki”.

Mwanamuziki ameongeza kwa kusema kuwa “iliniuma sana ingawa nilikuwa na umri mdogo na kila mara huwa natamani angeyaona mafanikio yangu,”.

Chemical ni moja wa marapa walioibuka hivi karibuni pamoja na kufanya vizuri katika kazi zake nyingi pia ameleta  changamoto kwa marapa wa kike waliomtangulia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *