Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Claudia Lubao maarufu kama Chemical amesema yeye bado ni mwanamke ambaye hajawahi kukutana na mwanaume yeyote ‘bikira’ na kwamba jimbo lake lipo wazi yaani yupo ‘single’.

Chemical ameongeza kusema anafurahi kuwa single ila mume wake ajaye ‘future hubby’ ata-enjoy sana kwa sababu anajua kupenda, muelewa na hatampangia vigezo vya mahari.

“Mahusiano ni kama unaishi na wazazi, utaulizwa kwa nini umechelewa, ulikuwa wapi… kwa hiyo mimi bado nipo single.

“Chemical ndio msichana pekee Tanzania mwenye hiyo sifa, mtoto bado mbichi off course, bikira kwani ni tusi? Sijaguswa, mtoto mlaini. Mtu akiamua kunioa nitamtunuku tu, sijaona sababu ya kutoa mahali sababu haitasaidia.

Kwa future hubby wangu namwambia ata-enjoy sana sababu Chemical ni mtu flani hivi anajua kupendwa anajua kupenda pia. Mimi nikikupenda uta-enjoy sana,,” amesema Chemical.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *