Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza imekubali ofa ya kumuuza kiungo wake Oscar kwenda klabu ya Shanghai SIPG ya China kwa ada ya uamisho itakayogharimu paundi milioni 60.

Kiungo huyo raia wa Brazil ataondoka kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Januari 12 mwakani.

Oscar amejiunga na Chelsea mwaka 2012 akitokea klabu ya Internacional ya nchini Brazil na kufanikiwa kushinda mataji ya ligi kuu Uingereza mara moja kombe la Ueropa ligi na kombe la ligi kwa kipindi cha miaka minne klabuni hapo.

Mchezaji huyo akuwa na nafasi katika kikosi cha kocha mpya Chelsea Antonio Conte baada ya kucheza mechi chache toka awasili kwa mtaliano huyo.

Kiungo huyo wa Brazil ataungana na aliyekuwa kocha wa Chelsa Andre Villas-Boas ambaye ndiyo kocha mkuu katika klabu ya Shanghai SIPG  .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *