Chelsea wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Manchester United kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la FA kwenye uwanja wa Stanford Bridge.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa hapo jana baada ya mechi hizo kumalizika katika raundi ya nne ambapo Manchester United waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Blackburn.

Mechi nyingine zitakuwa kama ifuatatvyo, Middlesbrough itakutana na kati ya Huddersfield na Manchester City, Tottenham itakutana na Millwall na Suton uso kwa uso na Arsenal au Lincoln.

Mechi ya mwisho kukutana kati ya Manchester United na Chelsea ikuwa mwaka jana ambapo Chelsea ilishinda 4-0 kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza.

Michezo hiyo ya robo fainali itachezwa kati ya tarehe 11 na 12 ya Mwezi Machi mwaka huu kulingana na ratiba hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *