Klabu ya Chelsea imepigwa faini ya euro 100,000 na Manchester City wamepigwa faini ya euro 35,000 baada ya wachezaji wao kuhusika katika vurugu uwanjani wakati wa mechi ya Ligi kuu.

Fujo hizo zilitokea baada ya Sergio Aguero wa Manchester City kutolewa uwanjani kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea visivyo beki wa Chelsea, David Luiz.

Pia Fernandinho alitolewa kwa kadi nyekundu uwanjani kwa kumkaba koo Cesc Fabregas kutokana na fujo uwanjani hapo.

Chelsea hapo awali wametahadharishwa kwamba wanaweza kupokonywa alama kwa utovu wa nidhamu.

Chelsea wamepigwa faini mara sita tangu Februari 2015 kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake wawapo uwanjani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *