Mwanamuziki wa Bongo fleva, Chege Chigunda amesema kuwa yeye hana bifu na mkali mwenzie Juma Nature kama inavyodhaniwa na mashabiki nchini.

Chege ambaye aliongozwa na Nature wakiwa TMK Wanaume Family kabla ya kundi hilo kugawanyika amekiri kuwa anaonana na Nature kwa nadra kutokana na changamoto za kimaisha kwani kila mmoja yupo bize kivyake.

Muimbaji huyo anayetamba na wimbo wake ‘Kelele za Chura’ amesema kuwa hawezi kuwa na bifu na Nature kutokana wote ni wanamuziki hivyo kufanya hivyo ni kujishusha kwenye tasnia ya muziki wa Bongo fleva.

Juma Nature
Juma Nature

Wawili hao walikuwa katika kundi moja miaka ya nyuma TMK Wanaume Family chini uongozi wa Said Fella lakini baadae wakaja kugawanyika kutokana na maslai ya kikazi hivyo Juma Nature akatoka na kuanzisha TMK Wanaume Halisi.

Toka kuvunjika kwa kundi hilo wawili hao hawajakutana kufanya kazi pamoja hadi sasa ndicho kinachopelekea mashabiki kusema wawili hao uhenda wakawa na tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *