Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na kutoonekana katika steji ya Bendi ya Mashujaa aliyokuwa akiifanyia kazi, mwanamuziki Chaz Baba ameeleza sababu za kupotea kwake.

Chaz Baba amesema alikaa kimya kwenye steji kwa kuwa alikuwa bize kufanya nyimbo zake binafsi na anatarajia kurejea kwa kishindo hivyo mashabiki wakae mkao wa kula.

“Nimekaa kimya kwenye steji kwa muda mrefu lakini hivi karibuni nitaachia wimbo wangu mpya unaitwa Nuru na nina nyimbo nyingine mpya 13 ambazo nitazitoa kwa utaratibu moja baada ya nyingine mpaka ziishe,”.

Pia mwanamuziki huyo amewataka mashabiki wampokee katika marejeo yake kama msanii anayejitegemea licha ya muziki wa bendi kushuka.

Mwanamuziki huyo alitamba na bendi mbalimbali kama vile Twanga Pepeta na Mashujaa Music Band ambayo kwasasa imepoteza makali yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *