Hatimaye klabu ya Chapecoense ya Brazil imeanza mazoezi ya kujiandaa kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini humo utakayonza Januari 26 mwaka huu wakicheza na Joinville uwanja wa nyumbani.
Klabu hiyo imesajili wachezadi 20 ili kuziba pengo baada ya wachezaji na vingozi wa timu hiyo kufariki dunia kwa ajali ya ndege iliyotokea nchini Colombia walipokwenda kucheza fainali ya kombe la Sudamericana dhidi ya Atretico Nacional ya Colombia.
Wachezaji tisa walipoteza maisha kwenye ajali hiyo ya ndege iliyotokea mwezi Novemba mwaka jana huku wachezaji wengine wakipona lakini wameachwa na ulemavu.
Chapecoense kwa sasa wameanza mazoezi na kusahau yote yaliyopit akwa wakijiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini Brazil ambao unatarajia kuanza Januari 26 mwaka huu kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Joinville.