Chalinze kujenga kiwanda cha Tiles

0
276

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameanza harakati za kujenga kiwanda cha Tiles katika jimbo lake ambacho kinaweza kuja kutoa ajira kwa watu zaidi ya elfu sita nchini.

Ridhiwan Kikwete amesema kazi yake ni kutafsiri malengo mema aliyonayo Rais John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo na kudai lengo kubwa la kujenga kiwanda hicho ni pamoja na kutoa ajira kwa vijana na wakina mama.

Mbali na hilo Mh Ridhiwan Kikwete amedai kiwanda hicho kikikamilika malighafi zake za uendeshaji wa kiwanda hicho zitakuwa zikitoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu, Pugu, Morogoro na Tanga na kusema zaidi ya asilimia 90 ya malighafi zitakuwa zikitoka hapa hapa Tanzania.

Mbunge huyo amesema kuwa malighafi Zitatoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu,Pugu, Morogoro, na Tanga.

 

 

LEAVE A REPLY