Klabu ya West Brom imemsajili kiungo wa Ubelgiji, Nacer Chadli kutoka Tottenham kwa ada ya uamisho ya paundi milioni 13 ambapo amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Tottenham akitokea klabu ya FC Twente ya Uholanzi mwaka 2013.

Chadli ameichezea Spurs mechi 119 na ameshinda magoli 25 tu lakini kwasasa ameonekana hana nafasi kwenye kikosi cha Muargentina Mauricio Pochettino msimu huu.

Nacer Chadli: Akishangilia goli lake kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza.
Nacer Chadli: Akishangilia goli lake kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza.

Baada ya kusajiliwa kwa mchezaji huyo West Brom inakuwa inatimiza jumla ya wacheza watatu kusajiliwa klabuni hapo kutokana na kufanya usajili wa Matt Phillips kutoka QPR pamoja na Brendan Galloway kutoka Everton kwa mkopo.

Mpaka sasa West Brom inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza baada ya kujikusanyia alama 4 pekee ambapo wameshinda mechi moja wamesuluhu moja na kufungwa moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *