Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kisitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike nchi nzima kesho Septemba Mosi yaliyopewa jina la UKUTA.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa wamefanya mazungumzo na viongozi mbalimbalia wakiwemo viongozi wa dini, BAKWATA, Baraza la Maaskofu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Taasisi ya Mwalimu Nyerere na Jukwaa la Katiba na Jukwaa la wahariri na kuona wana kila sababu ya kusikiliza ushauri huo.

Maandamano hayo yameahirishwa kwa mwezi mmoja ili viongozi wa dini kutafuta muafaka wa hali ya kisiasa nchini.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitangaza kwamba ifikapo Septemba 1 itakuwa siku ya maandano nchini nzima ambapo maandanamno hayo yalikuwa yakijulikana kama UKUTA.

Maandamano hayo yalikuwa yanapingwa vikali na baadhi ya watu nchini kutokana uenda yakasababisha uvunjifu wa amani nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *