Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza operesheni mpya walioipa jina la ‘Kata Funua’ kwa ajili ya kujiimarisha vijijini zaidi.

Opreresheni hiyo imetangazwa na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe katika uchaguzi wa cha chama hicho kanda ya kusini, kanda ya Masasi mkoani Mtwara.

Mbowe amesema kuwa operesheni hiyo ni sehemu ya maandalizi ya chama hicho kwa uchaguzi wa mwaka 2019/20 ambapo itatekelezwa kwa kufanya mikutano mikutano maeneo ya vijijini.

Kwa upande mwingine Mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Edward Lowasa aliwataka viongozi wa chama hicho kuimarisha umoja na mshikamano na kwamba mtu yeyote atakayetaka kuvuruga umoja huo achukuliwe hatua kali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *