Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema kuwa hawakubaliani na matokeo na ubunge wa Afrika Mashariki na wataenda Mahakamani kupinga matokeo hayo.

Hayo yamekuja baada ya wagombea wawili wa CHADEMA, Lawrence Masha na Ezekiel Wenje kutupwa nje baada ya kupigiwa kura za ‘HAPANA’.

Katika uchaguzi huo kulitokea mabishano ya kikanuni juu ya wagombea hao wa CHADEMA yaliyosabaishwa na chama hicho kuweka wagombea wawili pekee huku nafasi kwa ajili ya chama hicho zikiwa mbili pia.

Suala hilo lingewalazimu wapiga kura kupiga kura za kuwakubali wagombea hao hata kama hawawataki.

Spika Job Ndugai aliamua kura zipigwe, lakini kwa kundi la wagombea wa CHADEMA akaelekeza kuwa wapiga kura wa uhuru wa kuweka alama ya ‘tick’ kama wanamkubali mgombea au alama ya ‘X’ kama hawamkubali.

Wabunge hao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipiga kura na kuwachagua wajumbe 7 wa Bunge la Afrika Mashariki sita wakitoka CCM na mmoja akitoka CUF.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *