Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kumuunga mkono Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Kenya utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Msimamo huo umetolewa leo katika mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho unaofanyaki mjini Dodoma, ikiwa ni maamuzi ya Baraza hilo, na kutangazwa rasmi na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

Akizungumzia uamuzi huo, Mbowe amesema sababu kuu ya uamuzi huo ni kugeukwa na mgombea wa muungano wa ODM Raila Odinga, ambaye chama hicho kilikuwa kikimuunga mkono mara zote.

Mbowe amesema “Kwa muda mrefu chama chetu kimekuwa kikimuunga mkono Raila Odinga achukue nafasi ya kuliongoza Taifa la Kenya. Mwaka 2015 ilipofika zamu yetu rafiki yetu Raila Odinga alitugeuka na kumuunga mkono adui yetu. Sisi kama Chama, safari hii tunamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na Umoja wa vyama vinavyounda JUBILEE”.

Chama hicho kinaendelea na Baraza Kuu mjini Dodoma, baada ya hapo jana kumaliza kikao cha Kamati Kuu yake, na kimedhamiria kutoka na maamuzi mazito kuhusu mustakabali wa taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *