Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu anatarajiwa kukabidhiwa kadi ya Chadema akiwa pamoja na kundi lake lenye zaidi ya watu 500 waliojiunga na chama hicho wiki iliyopita.

Chadema wamesema kuwa wapo kwenye maandalizi ya mwisho ya kumkabidhi kadi mrembo ili aweze kuwa mwanachama hai wa chama hicho kikubwa cha upinzani hapa nchini.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene, amesema   wapo kwenye maandalizi na kabla ya Machi 5, mwaka huu watamkabidhi Wema kadi ya uanachama   na kundi lake linalomuunga mkono.

Wema alikuwa mmoja kati ya wanachama maarufu wa CCM katika kundi la wasanii wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka juzi kwa kaulimbiu ya ‘mama ongea na mwanao’.

Muigizaji huyo alishiriki kumnadi Mgombea Mwenza wa CCM ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Katika mkutano wake na wanahabari mwishoni mwa wiki,  Wema  alisema kwa sasa ameamua kuvaa magwanda na yupo tayari kwa mapambano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *