Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeamua kushusha chini zaidi madaraka kwa wanachama wake katika ngazi ya familia kwa njia ya kuanzisha mabalozi wa nyumba kumi kama ilivyo kwa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vincent Mashinji amesema kuwa chama hicho hivi sasa kimeamua kuzidi kujiimarisha katika ngazi ya familia, hivyo kugatua madaraka kutoka juu, kwenda katika ngazi ya kanda hadi mabalozi wa nyumba kumi.

Amesema hatua hiyo itarahisisha watu kukifahamu zaidi chama hicho pamoja na sera zake, pia itakuwa rahisi kutoa elimu ya uraia kuanzia ngazi ya familia, lakini pia itawawezesha viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini kuwa na uwezo wa kushughulikia harakati pamoja na matatizo yatakayokuwa yakijitokeza, na hatimaye kukiwezesha kushika dola katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Ameongezea kwa kusema kuwa  hivi sasa chama hicho kinafanya kazi kwa mikutano ya ndani, ambapo viongozi wote wakuu wa chama watapita kwenye kanda zote kufanya ukaguzi na ufuatiliaji, ili kuhakikiksha chama hicho kinakuwa na wanachama wapya, watakaokiwezesha kushinda katika kila uchaguzi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *