Mwanamuziki mkongwe kutoka Canada, Celine Dion amekanusha taarufa za kutoka kimapenzi na mcheza dansi wake Pepe Munoz.

Celine amekanusha tuhuma hizo kupitia mtu wake wa karibu baada ya picha  zake akiwa na kijana huyo mjini Paris kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Picha zilizagaa ziwaonyesha wawili hao wakiwa matembezi na wenye furaha na kufanya watu wajue kuwa ni wapenzi sio kweli bali ni watu wanaofanya kazi pamoja.

Pepe amekuwa akitumika  na Celion Dion katika matamasha yake ya kimuziki amekuwa na mchango mkubwa katika masuala ya mitindo kwa mawanamuziki huyo.

Picha zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii ziliwaonesha wawili hao wakiwa ni watu wenye furaha sana mpaka kupelekea kuhisi wawili hao uhenda wakawa katika mahusiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *