Chama cha Mapinduzi (CCM) kisema kuwa mabadiliko ya kimuundo na uendeshaji wa chama hicho kimepokelewa vizuri na wanachama wake.

Taarifa iliyotolewa leo kupitia kwa Katibu wa Katibu Mkuu wa CCM, bwana Charles Charles imeeleza kuwa mabadiliko hayo yamepokewa kwa shangwe ndani na wanachama wote wa chama hicho na wala hayamlengi mtu yoyote ndani ya chama.

 

Kuhusu ya kupunguza Wajumbe wa Kamati Kuu kutoka 34 na kubaki 24 na Wajumbe wa NEC kutoka 388 na kubaki 158, taarifa hiyo imesema imesema kuwa tangu kutangazwa kwa mabadiliko hayo siku ya Jumanne Desemba 13, 2016 hakuna mwanachama, kiongozi wala mfuasi yeyote wa CCM aliyelalamika, kuhoji au kunung’unukia mabadiliko yoyote yaliyopitishwa na vikao hivyo.

Pia kuhusu kuondolewa kwa nafasi kadhaa za ujumbe wa NEC chama hicho kimesema hakuna uhusiano wowote ule na madai ya rushwa ila ni mageuzi ya kawaida ndani ya chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *