Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa kinaridhishwa na utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Chama hicho kimesema kuwa Serikali imejikita zaidi katika kutekeleza Ilani ya Chama hicho ikiwemo kuipeleka Tanzania katika uchumi wa viwanda.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey PolePole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana.

Polepole amesema kuwa CCM imeridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya Tano kwani imefanya ziara ya uhakiki mkoa wa Pwani na kujionea ujenzi wa viwanda vikubwa, vya kati na vidogo.

Hata hivyo, PolePole amewaasa Watanzania kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *