Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amekiruhusu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kutumia ukumbi wao wa mikutano wa Jakaya Kikwete Hall uliopo Dodoma.

Kauli hiyo imetolewa na Polepole kufuatia mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe juu ya uwezekano wa chama hicho kutumia ukumbi huo.

Polepole amemwambia Mbowe kuwa CCM haioni uzito wa kutoa kibali kwa CHADEMA kutumia ukumbi huo ikiwa watawasilisha maombi rasmi kwa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.

Pia Polepole amemweleza Mbowe kuwa wataruhusiwa tu kuutumia ukumbi huo ikiwa watakubali masharti ya kutoweka alama za chama chao nje ya ukumbi huo isipokuwa sehemu ya ndani.

Tarehe 27 Mei 2017, CHADEMA watafanya Mkutano wa Kamati Kuu Mjini Dodoma na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho Boniface Makene haijabainisha ukumbi watakaotumka.

Upo uwezekano kuwa Mbowe ametekeleza masharti aliyopewa na huenda mkutano huo utafanyika ndani ya ukumbi wa CCM.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *