Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke, kimesema hakitamjadili Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, Yusuph Manji hadi kesi yake kuhusu madai ya kutumia dawa za kulevya itakapomalizika mahakamani.

Msimamo huo umetolewa baada ya kuwapo  taarifa kwamba chama hicho kimepanga kumjadili Manji kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.

Taarifa hizo zilieleza kuwa diwani huyo atajadiliwa vikaoni ili afukuzwe uanachama kwa kuwa chama hicho hakitaki wanachama wenye tuhuma na wanaovunja amri za nchi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema, alisema hawawezi kuingilia suala ambalo bado liko kwenye vyombo vya sheria.

Wiki iliyopita Manji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidaiwa kutumia dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *