Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya mkutano Mkuu maalum wa Taifa Machi 12 mwaka huu lengo likiwa ni kufanya marekebisho ya kanuni na katiba ya chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo amesema kuwa pamoja na mambo mengine mkutano huo pia utafanya kazi ya kujadili na kupitisha marekebisho ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2012 pamoja na kanuni za chama hicho na jumuiya zake.

Amesema pia mkutano huo utapokea taarifa ya ratiba ya uchaguzi Mkuu wa CCM na jumuiya zake utakaofanyika nchini kote mwaka huu wa 2017.

Mpogolo amesema marekebisho hayo ya katiba na kanuni za CCM na jumuiya zake yanafanyika kufuatia maamuzi ya Halmashauri kuu ya CCM yaliyofanyika mwezi Disemba 2016 mkoani Dar es Salaam.

Aidha mkutano Mkuu huo utatanguliwa na mikutano ya kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa itakayofanyika Machi 10 mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM ya Taifa utakaofanyika Machi 11 mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *