Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimepongeza utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli kwa mabadiliko aliyoyaleta serikalini na ndani ya chama.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,  Juma Simba  alipozungumza na waandishi wa habari ili kumpongeza Magufuli kwa jinsi alivyoendesha vikao vya CCM vilivyomalizika wiki chache zilizopita.

Bwana Simba amesema mabadiliko 23 ya chama hicho yaliyopitishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) jijini Dar es Salaam ambapo idadi ya wajumbe na idadi ya vikao vilipunguzwa ni jambo lenye ishara na nia njema.

Pia sekretarieti ya CCM iliyofanya vikao na mwenyekiti kuteua  nafasi zilizokuwa wazi baada ya waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ambao ni Humphrey Polepole aliyeteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa na Nape Nnauye ambaye sasa ni  Waziri wa  Habari.

Vile vile uteuzi mwingine ni Rodrick Mpogolo aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Bara akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Rajabu Luhwavi aliyeteuliwa kuwa balozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *