Wananchi wa jimbo la Catalonia wamepiga kura ya maoni kwa ajili ya kujiondoa kutoka nchi ya Uhispania.

Katika kura hizo asilimia 90 ya kura zilizopigwa jana katika eneo hilo zimeonesha kutaka kujitenga na nchi hiyo.

Hata hivyo Mahakama ya katiba nchini humo imedai kuwa, kura hizo zilikuwa kinyume na sheria.

Wakati wa upigaji kura ukiendelea watu takribani 844 walijeruhiwa katika maandamano yaliyotokea kati ya wananchi wa eneo la Cataluna na polisi wa usalama.

Kiongozi wa eneo hilo, Carles Puigdemont amesema kura hizo zimewapa haki watu wa eneo hilo baada ya mateso ya muda mrefu.

Kiongozi huyo ameongeza kwa kusema kuwa “Leo, siku hii yamatumaini na mateso pia, wananchi wa catalonia wameshinda haki ya kujitegemea kama taifa huru,” amesema kiongozi huyo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *