Kiongozi wa Catalonia, , Carles Puigdemont amesema kuwa jimbo hili litatangaza uhuru wake kutoka Uhispania siku chache zijazo.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu ifanyike kura ya maoni siku ya Jumapili, Carles Puigdemont amesema kuwa serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo.

Kwa upande wake mfalme wa Uhispania Felipe VI, amasema kuwa waandalizi wa kura hiyo walikiuka sheria ya nchi hiyo.

Maelfu ya watu kote eneo la Catalonia wamekuwa wakigoma kupinga ghasa za polisi wa Uhispania wakati wa kura, ambapo takriban watu 900 walijeruhwia.

Kiongozi huyo amesema kuwa serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzo wa wiki ijayo.

Alipoulizwa kuhusu ni kipi atakifanya ikiwa serikali ya Uhispania itaingilia kati na kuchukua udhibiti wa serikali ya Catalonia, Bw Puigdemont alisema kuwa yatakuwa ni makosa ambayo yatabadilisha kila kitu.

Puigdemont alisema kuwa sasa hakuna mawasiliano kati ya serikali mjini Madrrid na utawala wake.

Alipinga taarifa ya tume ya ulaya ya siku ya Jumatatu kuwa kile kinachoendelea Catalonia ni masuala ya ndania ya Uhispania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *