Muigizaji  maarufu nchini Marekani, Cassie ameamua kurudiana na mpenzi wake staa wa hip hop, P. Diddy baada ya kumwagana kwa ugomvi mzito siku chache zilizopita.

Taarifa ya kurudiana kwa wapenzi hao imetolewa na mtandao wa TMZ ambapo Cassie amebadili moyo wake na kurudi kwa Diddy rasmi na kumaliza tofauti zao.

Kwa mujibu wa TMZ chanzo cha ugomvi wao ulitokana na Cassie kumwambia Diddy kuwa anataka waachane bila sababu.

Cassie na Diddy
Cassie na Diddy

Kitendo hiko kilimkasirisha Diddy kiasi cha kushika simu na kuanza kuikagua na baadaye akaondoka nayo lakini baada ya muda alimrudishia Cassie simu yake.

Ugomvi huo uliwahusisha mpaka polisi wa Beverly Hills waliofika nyumbani kwa Cassie walioitwa na mama yake lakini hata hivyo aliwaeleza kuwa ameipata simu yake na wakaondoka japo waliandika ripoti ya tukio hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *