Golikipa wa Porto, Iker Casillas pamoja na wachezaji wa Chelsea, Cesc Fabregas na Pedro wameachwa kwenye kikosi cha kocha mpya wa timu ya taifa ya Uhispania, Julen Lopetegui.

Wachezaji, Diego Costa wa Chelsea na kiungo wa Manchester United, Juan Mata wameitwa kwenye kikosi hiko baada ya kuachwa kwenye michuano ya Euro iliyomalizika nchini Ufaransa.

Uhispania inatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ubelgiji pamoja na mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Liechtenstein mwezi Septemba.

Wachezaji wengine walioitwa kwenye kikosi hiko ambao wanacheza Uingereza ni David de Gea kutoka Manchester United, Adrian kutoka West Ham na beki , Cesar Azpilicueta kutoka Chelsea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *