Mshambuliaji wa Boca Junior ya Argentina, Carlos Tevez ameuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Vanesa Mansilla.

Ndoa ya mshambuliaji huyo wa zamani wa vilabu vya Manchester United na Manchester City imefanyika katika mji mkuu wa Argentina,  Buenos Aires na kuhudhuriwa na watu maarufu nchini humo.

Mshambuliaji huyo mtukutu amefunga ndoa na mpenzi wake huyo ambaye ameanza nae mahusiano toka mwanamke akiwa na umri wa miaka 13 katika mji huo maarufu wa Buenos Aires nchini Argentina.

carlos

Carlos Tevez na mke wake huyo wamejaliwa kupata watoto wawili Frorence na Katie wote wanawake.

Mshambuliaji huyo kwasasa anahusishwa kuhamia moja wapo ya klabu nchini China baada ya vilabu nchini humo kuonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *