Timu ya taifa ya Cameroon imefanikiwa kutinga fainali ya mataifa ya Afrika (Afcon) baada kuifunga Ghana 2-0 katika mechi ya nusu fainali iliyfanyika jana.

Timu zote mbili zilicheza mchezo wa kuvutia huku ikishuhudiwa kipindi cha kwanza zikimaliza kwa sare ya bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo milango ya kila timu iliendelea kuwa migumu mpaka dakika ya 72 Michael Ngadeu-Ngadjui alipofunga goli la kwanza kwa Cameroon.

Zikiwa zimesalia sekunde chache huku Ghana wakijaribu kusawazisha Christian Bassogog alifunga goli la pili na kuzamisha kabisa matumaini ya Ghana kwa mwaka huu.

Matumanini ya Ghana kuchukua kikombe hicho ambacho kwa mara ya mwisho walikibeba mwaka 1982 sasa yamefikia mwisho katika michuano ya mwaka huu.

Mara ya mwisho kwa Cameroon kuingia fainali ilikuwa mwaka 2008 walipofungwa na Misri ambao ndio wanakutana nao tena katika fainali ya mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *