Timu ya Taifa ya Cameroon imeibuka bingwa wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa kuifunga Misri 2-1.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Misri walikuwa mbele kwa goli moja lililofungwa na Mohammed Elneny katika dakika ya 22 ya mchezo huo.

Cameroon walisawazisha goli lake katika dakika ya 59 kupitia beki wake Nkoulou baada ya kupiga kichwa na kumshinda kipa wa Misri, El Hadary.

Goli la ushindi la Cameroon kwenye mechi hiyo limefungwa na mshambuliaji wake Vicente Abubakar katika dakika ya 88 ya mchezo huo.

Misri ambayo ilikuwa imenuia kushinda mashindano hayo na kuweka rekodi ya mshindi mara nane, ilikuwa ikiongoza katika kipindi cha kwanza.

NI mara ya tano kwa Cameroon kubeba kombe hilo ya mataifa ya Afrika na mara yake ya mwisho tangu mwaka 2002.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *