Mwanamitindo maarufu nchini, Calissa amesema kuwa alitengwa na familia yake baada ya picha zake na Wema Sepetu kusambaa mitandaoni miezi kadhaa iliyopita.

Calissa amesema kuwa amezaliwa kwenye familia yenye kumcha Mungu lakini hajafika Msikitini zaidi ya miaka 5 kwasasa japokuwa ni muislam.

Mwanamitindo huyo amesema kuwa baada ya picha kusambaa akiwa na Wema Sepetu taarifa ziliifikia familia yake wakati akiishi na Bibi yake ambaye ni sala tano ambapo taarifa zilimfikia Bibi yake kwamba mjukuu wake anacheza picha za ngono.

Wema Sepetu
Wema Sepetu

Kutokana na taarifa hizo Bibi yake presha ikapanda  na umauti ukamfika, ndipo familia ambayo Shangazi na wajomba wakamtenga.

Muda huu Callisa amefungua kampuni anamiliki video vixen 100, ukitaka video Queen unaona naye pia anakodishi magari kwa ajili ya kufanyia video.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *