Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) leo limetoa orodha ya wachezaji watakaocheza Fainali za Vijana chini ya miaka 17 (U17) zitakazoanza kutimua vumbi wikiendi hii nchini Gabon.

CAF imetangaza orodha ya wachezaji 21 kwa kila nchi mshiriki zinazoshiiriki mashindano hayo yatakayoanza Mei 14-28 nchini Gabon, huku timu nne za juu zikipata nafasi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia baadae mwaka huu nchini India.

Kikosi cha Serengeti Boys kinajumuisha magolikipa watatu,  walinzi  nane, viungo  sita ma washmabuliaji wanne.

Michuano hiyo inashiriikisha nchi 8 zilizo katika makundi mawili ambapo kundi A kuna wenyeji Gabon, Cameroon, Ghana na Guinea, huku kundi B kukiwa na mabingwa watetezi Mali, Tanzania, Angola na Niger.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *