Serikali ya Burundi inayoongozwa na rais Perre Nkurunzinza imetangaza dhamira yake ya kujiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya makossa ya uhalifu dhidi ya binadamu ya ICC.

Baraza la mawaziri la Burundi limefikia uamuzi huo usiku wa jna kufuatia kikao maalum kilichokaliwa kujadili masuala ya usalama ya nchi hiyo.

Kauli hiyo imekuja miezi sita baad aya mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo atangaze kuwa ofisi yake itaanza uchunguzi wa vurugu zilizotokea nchini humo mwaka jana na kusababisha vifo vya mamia ya watu.

Mahafuko ya kisiasa yalizuka tena nchini Burundi mwaka jana kufuatia tangazo la rais Pierre Nkurunzinza alilolitoa mwezi wa Aprili mwaka 2015 kudai kuwa atawania uongozi wa kiti hicho kwa awamu ya tatu.

Huku bunge la nchi hiyo likisubiriwa kupitisha muswada huo wa kujitoa ICC, makamu wa rais wan chi hiyo Gaston Sindimwo amesema kuwa serikali ya Burundi haina hofu na uamuzi wowote wa kimataifa utaochukuliwa dhidi yao huku akiamini kuwa nchi hiyo itatengwa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *