Timu ya Taifa ya Burkina Faso imefanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Afcon baada ya kuifunga Ghana 1-0 kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa Port-Gentil.

Goli pekee katika mechi hiyo limefungwa na Alain Traore katika dakika ya 89 baada ya kupiga faulo na kumshinda kipa wa Black Stars, Richard Ofori na kutinga kimiani na kuifanya Burkina Faso kutwaa nafasi hiyo.

Ghana ilitolewa na Cameroon katika hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kipigo cha 2-0, huku Burkina Faso ikiondoshwa na Mafarao wa Misri kwa njia ya mikwaju ya penalti.

Fainali ya michuano hiyo itafanyika leo kati ya Cameroon na Misri ikiwa ni marudio ya fainali ya mwaka 2008 nchini Ghana.

Misri ni mabingwa wa kihistoria wa Afcon kwa kuwa wametwaa taji hilo mara saba, huku Cameroon maarufu kama wakitwaa ubingwa huo mara nne.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *