Bunge nchini Cuba limepitisha katazo la kuzuia majengo, mitaa au minara ya kumbukumbu kupewa jina la mwanamapinduzi mkongwe nchini humo Fidel Castro ambaye alifariki dunia mwezi uliopita.

Mwanamapinduzi huyo alikataa kwa maeneo mbali mbali nchini humo kutiwa jina lake kama kumbu kumbu akitaka wamkumbuke kwenye mawazo yao na siyo kwenye maeneo nchini humo.

Fidel Castro aliongoza mapinduzi ya Cuba, ambayo mwaka 1959, waliuondoa madarakani utawala uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani.

Aliifanya nchi hiyo kuwa ya Kikomunisti na kubaki kwenye utawala kwa takriban miongo mitano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *