Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema kuwa atafungua kesi ya madai dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo Stephen Wasira (CCM).

Bulaya amesema hayo wakati wa mkutano wake na wananchi wa jimbo la Bunda Mjini kwa mara ya kwanza toka ashinde kesi katika mahakama ya rufaa jijini Dar es Salaamm dhidi wa Wasira.

Katika mkutano wake huo na wananchi mbalimbali wa Bunda mkoani Mara wananchi hao walitaka kujua Bulaya kama atamsamehe Wasira au atamdai fidia kutokana na kesi iliyochelewesha maendeleo ya wananchi wa Bunda.

Bulaya amesema kuwa watafungua kesi ya madai ili afanikishe maendeleo ya watu wa Bunda kutokana na kutenga milioni 20 kata 7 zote za mjini kwa ajili ya kusambambaza mabomba ya maji ili kuondoa shida ya maji.

Kwa upande wa wananchi wa Bunda wamemtaka mbunge wao kudai fidia dhidi ya kesi iliyokua inamkabili kufuatia Wasira kufungua kesi na kusema kuwa ushindi wa Bulaya haukua halali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *