Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (CHADEMA) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akitibiwa tangu wiki iliyopita baada ya afya yake kuimarika.

Bulaya alikamatwa na polisi Ijumaa, Agosti 18 akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime mkoani Mara akidaiwa kutaka kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria ambapo aliswekwa rumande.

Hali ya Mbunge huyo ilibadilika ghafla siku iliyofuata baada ya presha kupanda, hivyo kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime ambapo baadaye alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo Mwanza, kabla ya kusafirishwa kulazwa wodi namba 18 katika jengo la Sewahaji akipatiwa matibabu.

Baada ya kutoka hospitali mbunge huyo amesema kuwa “Kwanza nitapumzika kwa siku 10, hivyo ndivyo nilivyoagizwa na nitatakiwa kurudi tena hospitalini kwa ajili ya kuangaliwa afya yangu zaidi.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Kwa sasa nitapumzika kabla ya kurudi jimboni kuendelea  na shughuli za maendeleo,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *