Mahakama ya Rufani imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na wapiga kura 4 wa Jimbo la Bunda Mjini kupinga ushindi wa Mbunge, Esther Bulaya.

Shauri hilo lilifunguliwa na Magambo Masato na wenzake wanne, wakiiomba mahakama kutengua matokeo yaliyompa ushindi mbunge Ester Bulaya (CHADEMA).

Miongoni mwa madai ya msingi ya walalamikaji yaliyowasilishwa mahakamni wakiwakilishwa na mawakili wawili, Constatine Mutalemwa na Denis Kahangwa, walidai aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Stephen Wasira alikataliwa ombi la kuhesabu wala kuhakiki kura baadhi ya vituo, kuwapo mianya ya rushwa na kunyimwa haki yao ya kuchagua.

Baada ya ushindi huo Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya ameandika ujumbe huu: Wana Bunda wameshinda tena na tena, asante Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *