Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amefunguka sababu ya kukamatwa na kupoteza fahamu akiwa mahabusu na kupelekea kulazwa hospitali kwa matibabu.

Bulaya kwa mara ya kwanza ameelezea kile kilichojiri akiwa mahabusu mpaka kupelekea kupoteza fahamu na kulazwa.

Pia Bulaya amesema kuwa sababu ya kukamatwa kwake ilikuwa kwa kosa la kwenda kutoa misaada kwenye shule iliyopo kwenye jimbo la mbunge mwenzake wa CHADEMA John Heche.

Bulaya akiwa hospitali wakati alipolazwa baada ya kupoteza fahamu akiwa mahabusu.
Bulaya akiwa hospitali wakati alipolazwa baada ya kupoteza fahamu akiwa mahabusu miezi kadhaa iliyopita.

Mbunge huyo ameendelea kusimulia kwamba baada ya kumkamata akawaambia kwamba ana tatizo la pumu, hivyo wasimuweke kwenye mazingira ambayo yanaweza yakamletea matatizo kiafya, lakini wakamuingiza mahabusu bila kujali afya yake.

Baada ya muda hali ikaanza kubadilika, na ndipo mahabusu wenzake aliokuwa nao ndani wakaanza kupiga kelele wakiwa ndani ili polisi waje wasaidie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *