Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ameliomba bunge la nchi hiyo kumuongezea likizo yake ya kupata matibabu nchini Uingereza.

Ametoa taarifa hiyo akiwa nchini Uingereza kwa ajili ya vipimo vya afya yake alivyofanyiwa nchini humo.

Buhari aliondoka nchini Nigeria wiki mbili zilizopita na alitarajiwa kurudi mjini Abuja jana lakini ikashindikana kutokana na hali yake kutokuwa nzuri.

Taarifa iliyotolewa na ofisi yake imesema ameshauriwa na madaktari kumaliza matibabu na kusubiri matokeo ya vipimo alivyopima.

Kiongozi huyo aliomba likizo kwa kwa ajili ya matibabu kutokana na kusumbuliwa mara kwa mara hivyo akaomba ruhusa kwa bunge la Nigeria ili kwenda kupata matibabu nchini Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *