Mwanamuziki kutoka Kenya, Fredrick Mutinda ‘Brown Mauzo’ ameweka wazi kuwa kabla ya kutoka kimuziki Wakenya wengi walikuwa wakimuona na kumsikia tofauti na kudhani huenda ni Mtanzania.

Mauzo anayetikisa kwa sasa na Ngoma ya Nitulize alioshirikiana na Ali Kiba pia alizima tetesi zilizokuwa zikizagaa kuwa alikuwa na bifu na Ali Kiba kisa kikiwa ni kumgomea kufanya naye kolabo.

Brown Mauzo ambaye awali alikuwa akiishi Mombasa kwa sasa amehamishia makazi yake jijini Nairobi. Aliwahi kufanya kolabo Bongo na mastaa kibao wakiwemo, Rich Mavoko na Bob Junior.

Mwanamuziki huyo amefananisha na raia wa Tanzania kutokana na rafudhi ya lugha yake kufanana na ya kitanzania kutokana na mahali anapotokea katika mji wa Mombasa ni tofauti na watu kutoka Nairobi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *