Wiki iliyopita msanii Diamond Platnumzalikiri kufurahishwa na kitendo cha mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu kutoa sapoti kwa msanii Rich Mavoko.

Kitendo cha miss Tanzania (2006) kutoa sapoti hiyo kwa msanii aliye chini ya lebo ya WBC iliyo chini ya Diamond Platnumz kingeweza kuleta tafsiri mbalimbali miongoni mwa wafuatiliaji wa matukio ya wasanii wa Bongo lakini kitendo cha

Diamond kumshukuru Wema Sepetu hadharani kimechangia kuzima tetesi hasi ambazo zilianza kuvujishwa.

Ujasiri wa Wema wa kuweka mapenzi yake kwenye kazi mpya ya Rich Mavoko ni ushahidi tosha kuwa ‘MZALENDO hafungwi na mitazamo’……Kitendo cha Wema kuupenda wimbo wa Mavoko tu, kilimsahaulisha Wema juu ya tofauti zake na bosi wa msanii huyo.

Huenda kauli za wawili hawa zikafungua ukurasa mpya wa maisha yasiyo na uhasama.

Wakarudisha urafiki wao (wa kawaida) huku kila Mmoja akiendelea na maisha yake (ya kimahusiano) bila kumbugudhi mwenzake.

Sepetu

Congratulations Wema! You called a spade a spade!

Congratulations Diamond!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *