Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uteuzi wa kuwania urais kwa chama cha Democratic, Bernie Sanders ametangaza rasmi kumuunga mkono mpinzani wake Hillary Clinton.

Sanders ameutangaza uamuzi huo muda mfupi uliopita na anatarajiwa kuambatana na Clinton kwenye kampeni kwenye jimbo la New Hampshire.

Hillary Clinton anatarajia kutangazwa rasmi na chama cha Democratic kuwa mgombea wa nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Marekani ambapo anatarajiwa kuchuana na mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump.

Bernie Sanders: Aliyekuwa mpinzani wa Hillary Clinton
Bernie Sanders: Aliyekuwa mpinzani wa Hillary Clinton

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *