Hatimaye sintofahamu ya nani kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza baada ya kung’atuka kwa David Cameron imetatuliwa usiku huu kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kumtaka Bi. Theresa May kuunda Serikali mpya ya nchi hiyo.

Bi. Theresa May amekabidhiwa jukumu hilo kufuatia kujiuzuru rasmi kwa aliyekuwa mtangulizi wake, David Cameron.

Bw. Cameron aliwasilisha rasmi barua ya kuachia ngazi muda mfupi uliopita kwenye kasri ya Malkia huko Buckingham.

Muda mfupi baadae, Bi. Theresa alikutana na malkia Elizabeth II na kukabidhiwa jukumu hilo.

Bi. Theresa amekuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo nchini humo akitanguliwa na Margaret Thatcher.

Theresa May: Waziri mkuu mpya wa Uingereza
Theresa May: Waziri mkuu mpya wa Uingereza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *