Mtu anayedhaniwa kuwa mpiganaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabab ambaye alikuwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha Kapenguria kilichopo magharibi mwa Kenya, amepora bunduki na kuwaua askari kadhaa kisha kuwashikilia mateka maofisa wengine wa usalama kwenye kituo hicho.

Inspekta Jenerali wa Polisi, Joseph Binnet amekiri kutokea kwa tukio hilo na kudai jaribio la mtuhumiwa huyo la kutoroka limedhibitiwa baada ya msaada wa maafisa wa usalama kufika kwenye eneo hilo haraka.

Inadhaniwa kuwa zaidi ya askari watano wamepoteza maisha kwenye tukio hilo na wengine kadhaa bado wanashikiliwa mateka.

Shambulizi: Kikosi cha uokoaji cha Kenya kimetumwa kudhibiti shambulizi kwenye kit cha Polisi cha Kapenguria
Shambulizi: Kikosi cha uokoaji cha Kenya kimetumwa kudhibiti shambulizi kwenye kituo cha Polisi cha Kapenguria na kuwaokoa mattock

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *